Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LRA yafanya uvamizi zaidi kwenye Afrika ya kati

LRA yafanya uvamizi zaidi kwenye Afrika ya kati

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa limepokea ripoti za uvamizi unaoendeshwa na kundi la Lord’s Resistance Army LRA kwenye eneo la Afrika ya Kati.

Tangu machi 6 kumeripotiwa uvamizi mara 13 uliofanywa na LRA kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Watu wawili waliuawa na wengine 13 kutekwa nyara akiwemo mtoto kwenye mji wa Aba.

Uvamizi huo pia umewalazimu watu 1,160 kuhama makwao katika eneo la Dungu huku kukiwa na ripoti za uvamizi unaofanywa  na kundi hilo kutoka Uganda kwenye eneo la Bondo lililo karibu na mpaka na Jamhuri ya Afrika ya kati.

LRA inaripotiwa kufanya uvamizi mara 11 kwenye maeneo yaliyo kusini Mashariki mwa nchi  mwaka huu amnbapo watu wanne waliuawa kwenye uvamizi huo na 31 kutekwa nyara.

Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)