Mkurugenzi Mkuu wa IOM kuhutubia kongamano la kimataifa Dubai

Mkurugenzi Mkuu wa IOM kuhutubia kongamano la kimataifa Dubai

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM William Lacy Swing anatazamia kutoa hotuba maalumu wakati wa uzinduzi kongamano la kimataifa la misaada ya usamaria mwema huko Dubai.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa msaada mkubwa wa makamu wa rais na waziri mkuu wa Jumuiya ya falme ya kiarabu Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum.

Kongamano hilo la siku tatu ambalo litafunguliwa April 1, linatazamiwa kuwaleta pamoja viongozi mbalimbali wa dunia, wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na wawakilishi wengine kutoka sehemu mbalimbali.

Mwaka huu kongamano hilo linazingatia zaidi kuangalia nafasi za vijana kwenye utoaji misaada ya kibinadamu na maendeleo.

Litangalia kwa kina nafasi ya vijana katika maeneo yaliyokumbwa na vita na maisha baada ya vita.