Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China inaongoza kwa kusafirisha nje na kuingiza bidhaa za teknolojia ya mawasiliano

China inaongoza kwa kusafirisha nje na kuingiza bidhaa za teknolojia ya mawasiliano

Kwa mara ya kwanza Uchina sio tuu ni msafirishaji mkubwa anayeongoza kwa bidhaa za teknolojia ya mawasiliano (ICT) kama kompyuta na simu za mkononi bali tangu mwaka 2010 imekuwa ni muingizaji mkubwa wa bidhaa hizo.

Takwimu mpya za shirika la Umoja wa mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD zinaonyesha kwamba Uchina au Hong Kong ni sehemu zinazoongoza katika maeneo saba kati ya 10ambayo ni wasafirishaji wakubwa wa bidhaa za teknolojia ya mawasiliano.

Takwimu hizo za UNCTAD zinaungana na zile za mashirika mengine zilizotolewa kati ya mwaka 2000 na 2010.

Takwimu hizo zinaonyesha kwamba mataifa yanayoendelea yanachukua nafasi kubwa katika biashara ya bidhaa za teknolojia ya mawasiliano na kwamba sekta hiyo imeonyesha kutoyumba wakati wa mdororo wa kiuchumi duniani.

Takwimu hizo pia zinasema vifaa kama kompyuta, simu za mkononi za kisasa, vipaza sauti, televisheni na vifaa vingine vya sauti wakati wa msukosuko wa kiuchumi mwaka 2008 ndivyo vilivyopata mafanikio makubwa katika biashara kuliko sekta zingine za kichumi.

Mwaka 2010 Uchina imesafirisha vifaa vya ICT vya thamani ya dola bilioni 460, Hong Kong dola bilioni 177 huku Marekani ikisafirisha bidhaa za dola bilioni 135 tuu kati ya mwaka 200 na 2010.