Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kuzuru Chad na Niger

29 Machi 2012

Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang, Jumapili ataanza ziara ya siku sita nchini Chad na Niger kujadili  na serikali na wadau wengine masuala mbalimbali ya haki za binadamu.

Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kuzuru nchi hizo mbili na inakuja miezi sita baada ya ofisi ya haki za binadamu kupelekwa kundi la ushauri la haki za binadamu nchini Chad.

Bi Kang ataanzia N’Djamena Chad Aprili Mosi hadi tatu.

(RIPOT YA GRACE KANEIYA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter