Upungufu wa mafuta waweka maelfu ya wagonjwa hatarani Gaza:ICRC

Upungufu wa mafuta waweka maelfu ya wagonjwa hatarani Gaza:ICRC

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalama mwekundu ICRC inajiandaa kuipelekea wizara ya afya ya Gaza lita 150,000 za mafuta aina ya diesel.

ICRC inasema mafuta hayo yatasaidia kuendesha huduma muhimu katika hospitali 13 za umma katika siku 10 zijazo.

Kamati hiyo ilipeleka tena mafuta Gaza mwezi wa Februari.

Kwa mujibu wa mkuu wa ICRC Juan-Pedro Schaerer mwezi zaidi ya mmoja umepita tangu kuanza kwa matatizo ya mafuta na umeme Gaza na amesema kushindwa kuhakikisha huduma hizo zinapatikana kutaingilia huduma muhimu za jamii kama hospitali na maji na kuyaweka maisha ya maelfu ya wagonjwa hatarini.

Amesema ICRC imeshaonya kwamba uingiliaji wa aina yoyote wa huduma za hospitali hasa katika huduma za dharura na vitengo vya upasuaji na wodi za kujifungua kunaweza kuleta athari kubwa sana.

Ametaka hatua za haraka zichukuliwe na serikali na malka husika ili kuzia hali kuwa mbaya zaidi na kutafuta suluhu ya muda mref ya tatizo hilo.