Bodi ya kimataifa yakutana kukomesha biashara haramu ya bidhaa za tumbaku

29 Machi 2012
Mkutano wa kimataifa unaofanyika mjini Geneva umeamua kuongeza muda wa bodi ya kimataifa ya majadiliano INB kwa lengo la kumalizia awamu ya mwisho ya mkutano unaokamilisha mswada wa sheria ya kukomesha biashara haramu ya bidhaa za tumbaku.

Mkutano huo pia umeanzisha kundi lisilo rasmi la kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kabla ya kikao cha mwisho cha bodi ya kimataifa.

Kikao cha tano na cha mwisho cha bodi kimeanza Alhamisi Machi 29 na kitakamilika Aprili 4 mwaka huu.

Dr Haik Nikogosian ni mkuu wa secretariat ya mkataba kwenye shirika la afya duniani WHO.  

(SAUTI YA DR HAIK NIKOGOSIAN)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter