Mkuu wa UNIFIL na maafisa wa Israel na Lebanon wakutana

29 Machi 2012
Mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon UNIFIL na maafisa wa kijeshi wa Lebanon na Israel wamekutana kujadili masula muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama ambalo lilimaliza vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na kundi la Lebanon lijulikanalo kama Hizbollah.

Kwa mujibu wa mkuu wa UNFIL Meja jenerali Paolo Serra mkutano huo uliofanyika katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Ras Al Nagoura kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili ulikuwa wa mafanikio.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter