Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO na serikali ya Australia waanzisha mradi wa dola millioni 31 Timor-Leste

ILO na serikali ya Australia waanzisha mradi wa dola millioni 31 Timor-Leste

Shirika la kazi duniani ILO na serikali ya Australia wametangaza mradi mpya utakaogharimu dola milioni 31 kusaidia kuboresha usafiri wa barabara nchini Timor-Leste.

Ukifadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo la Australia AusAID mradi huo wa miaka mine moja ya miradi mikubwa kabisa ya maendeleo ya miundombinu katika eneo la Asia-Pacific. Mradi huo unatekelezwa na wizara ya miundombinu ya Timor-Leste kwa msaada wa kiufundi unaotolewa na shirika la ILO.

Pande hizo tatu yani serikali ya Timor-Leste, Australia na ILO wametia saini kuanza kwa mradi huo Alhamisi Machi 29 katika hafla maalumu iliyofanyika mjini Dili.