Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yaongezwa muda wa kuhudumu nchini Afghanistan

UNAMA yaongezwa muda wa kuhudumu nchini Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umesema kuwa kuongezwa kwa muda wake wa kuhudumu nchini Afghanistan kunatoa fursa ya kushirikiano na serikali ili kuleta amani, maendeleo na malengo mengine nchini humo. Juma lililopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililiongeza muda wa kuhudumu kwa UNAMA kwa mwaka mmoja zaidi ili iendelee kulisaidia taifa hilo wakati inapofanya mikakati ya kuboresha usalama wake.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan na mkuu wa UNAMA Jan Kubis amesema kuwa serikali ya Afhanistan inachukua umiliki wa mipango yote ya nchi hiyo. Ameongeza kuwa UNAMA itaendelea kuhakikisha kuwepo uwiano na amani na kutoa usaidizi kwa serikali.