Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana mkimbizi wa Kisomali ana ndoto ya kuwa nyota wa hip hop

Kijana mkimbizi wa Kisomali ana ndoto ya kuwa nyota wa hip hop

Saber ni kijana mkimbizi kutoka Somalia mwenye umri wa miaka 17 ambaye ana kipawa cha uimbaji wa nyimbo mtindo wa hip hop.

Hata hivyo Saber anasema kuwa bila ya kuungwa mkono na familia yake ndoto yake haitafanikiwa.

Kijana huyo kwa sasa amekwama kwenye kituo cha kupitishia wakimbizi cha Choucha karibu na mpaka kati ya Tunisia na Libya kwa karibu mwaka mmoja sasa akingonjea kwa hamu iwapo serikali ya Marekani nyumbani mwa muziki wa hip hop itampa makao ili apate kuendeleza kipawa chake.

Saber aliikimbia Somalia miaka mitano iliyopita na kuingia nchini Libya kabla ya kuikimbilia Tunisia mwezi Machi mwaka uliopita baada ya kuangushwa kwa serikali ya rais Muammar Gaddafi.