Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM aelezea Baraza la Usalama changamoto zilizoko nchini Guinea-Bissau

Mjumbe wa UM aelezea Baraza la Usalama changamoto zilizoko nchini Guinea-Bissau

Mjumbe wa UM nchini Guinea-Bissau amesema kipindi cha mpito cha sasa nchini ni moja ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

Joseph Mutaboba ameliambia Baraza la Usalama kuwa tangu kifo cha rais Malam Bacai Sanha, suala la kurejesha katiba kamili katika taifa hili la Afrika Magharibi limepewa kipaumbele muhimu.

Uchaguzi wa urais ulifanyika mapema mwezi huu, na kurejelewa kwa uchaguzi kati ya wagombea wawili wa urais umepangwa kufanyika mwezi April. Uchaguzi wa wabunge utafanyika baadaye mwaka huu.

(SAUTI YA JOSEPH MUTABOBA)

Guinea Bissau pia inakabiliwa na changamoto zinazohusiana na biashara haramu ya wadawa ya kulevya.

Mutaboba ameelezea changamoto zilizoko katika vita hii, ikiwa ni pamoja na matatizo ya fedha na kuzorota kwa mfumo wa mahakama.