Ofisi ya UM yahofia hatma ya watu wanaoishi kwenye kambi nchi Haiti huku msimu wa mvua ukiendelea

28 Machi 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa huku msimu wa mvua ukiendelea nchini Haiti hadi watu 65,000 wanaoishi kwenye kambi kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya mafuriko.

OCHA inasema kuwa tayari mvua zinazoendea kunyesha zimesababisha uharibifu kwa kambi tano kwenye mji mkuu Port-au-Prince.

OCHA inalalamika kuwa haikupata ufadhili wa kutosha kutokana na ombi ilililotoa mwaka huu.

Inasema kuwa imepokea chini ya asilimia kumi kati ya dola milioni 231 ilizoitisha.

Wakati huo huo kamanda mpya wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti  MINUSTAH amechukua wadhifa huo . Akiongea na Radio ya Umoja wa Mataifa jenerali Fernando Rodrigues Goulart amesema kuwa matarajio yake ni makubwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter