Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ESCAP kuisaidia Afghanistan kutoka kwenye vita na kuingia katika maendeleo

ESCAP kuisaidia Afghanistan kutoka kwenye vita na kuingia katika maendeleo

Umoja wa Mataifa uko tayari kuisaidia Afghanistan katika kipindi cha mpito kutoka vitani na kuingia katika maendeleo, hasa kwa kuisaidia kuiunganisha na mikakati ya maendeleo ya kikanda amesema Katibu Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii kwa ajili ya nchi za Asia na Pacific ESCAP.

Bi Noleen Heyzer akizungumza katika kongamano la kimataifa mjini Dushambe Tajikistan amesema Afghanistan ni muhimu na hatma yake inamanufaa kwa Asia Pacific na dunia kwa ujumla.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa kiuchumi na wa kikanda ni kiungo muhimu cha kuhakikisha utulivu na matumaini ya baadaye ya Afghanistan.

Kongamano hilo lililoanza Machi 26 limekuwa likijadili njia za kuchagiza amani, utulivu na matarajio ya Afghanistan.