UM umejidhatiti kuhakikisha usalama na utulivu Kuwait:Ban

28 Machi 2012
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema Umoja wa Mataifa umejidhatiti kuhakikisha kuna usalama na utulivu nchini Kuwait na kwamba kuna kuwa na utekelezaji wa maazimio yote ya Baraza la Usalama ikiwemo kutoweka kwa watu na mali nchini humo, mradi wa mpaka baina ya Kuwait na Iraq na ulipaji wa fidia.

Akizungumza mjini Kuwait City katika ziara ya siku moja Ban amegusia pia suala la Syria na kusema bado linatoa mashaka kutokana na machafuko yanayoendelea .

Ameongeza kuwa mchakato wa amani ya Mashariki ya kati bado uko hatarini akiwatolea wito viongozi wa Israel na Palestina kuenyesha ujasiri na mtazamo bora na kurejea kwenye majadiliano ambayo yatatatua masuala muhimu ya vita na kumaliza hali ya kukaliwa kwa Palestina iliyoanza mwaka 1967.

Amesema kwa niaba ya Umoja wa Mataifa anaahidi msaada kwa Kuwait kutekeleza maazimio.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter