Matukio ya hali mbaya ya hewa yanatarajiwa kuongezeka:IPCC

28 Machi 2012

Matukio ya kiwango cha juu na ya mara kwa mara ya hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya majira kama joto la kupindukia, mafuriko na ukame yanatarajiwa kuongezeka duniani kote kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa imesema ripoti mpya ya jopo la kimataifa la mabadiliko ya hali ya hewa IPCC.

Ripoti hiyo hata hivyo inasema imebaini kwamba kuna juhudi kidogo sana za kukabiliana na hatari zinazohusiana na majanga ya hali ya hewa, licha ya ufahamu uliopo kuhusu hali hizo.

IPCC inasema sera za kuepuka, kujiandaa, kukabiliana na kujikwamua na hatari ya majanga zinaweza kusaidia kupunguza athari za matukio ya hali mbaya ya hewa na kuwafanya watu walio katika hatari kuwa makini zaidi.

(SAUTI YA DR. PACHAURI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter