Pillay apongeza uchaguzi wa Senegal na kuzitaka Mali na Guinea Bissau kufuata nyayo

28 Machi 2012
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay Jumatano ameipongeza Senegal kwa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais kwa amani, uhuru, haki na kwa uwazi, na amezitaka nchi zingine katika kanda hiyo kufuata nyayo.

Pillay amesema katika wakati ambao kuna ghasia zinazoambatana na uchaguzi katika sehemu zingine za Afrika ya Magharibi inatia moyo kuona watu wa Senegal, wajumbe wa vyama vya siasa, jumuiya za kijamii na wadau wengine kwa pamoja wamehakikisha wanafuuata utamaduni wa nchi hiyo wa amani na kubadilishana madaraka kwa njia ya kidemokrasia.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter