Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lazitaka Sudan na Sudan kusini kujizuia kuendeleza machafuko mpakani

Baraza la Usalama lazitaka Sudan na Sudan kusini kujizuia kuendeleza machafuko mpakani

Baraza la Usalama limetoa tahadhari kuhusu mapigano ya kijeshi kwenye maeneo ya mpakani kati ya Sudan na Sudan Kusini, likisema makabiliano hayo yanatishia kuchochea vita baina ya nchi hizo mbili, kuzorotesha zaidi hali ya kibinadamu na kusababisha vifo vya raia.

Wajumbe wa Baraza la Usalama wamezitaka Sudan na Sudan Kusini kujizuia na kufanya mazungumzo ya amani ili kushughulikia masuala ambayo yamechangia kutoaminiana baina yao ikiwemo tofauti kuhusu mafuta, machafuko kwenye jimbo la mpakani, uraia na mvutano dhidi ya eneo la Abyei.

Kwa niaba ya wajumbe balozi wa uingereza kwenye Umoja wa Mataifa Mark Lyall Grant ambaye ndiye Rais wa Baraza la Usalama mwezi huu amesema wajumbe wa baraza wamezitaka Sudan na Sudan Kusini kuheshimu mkataba wa maelewano waliotia saini Februari 10 unaopinga machafuko na kudumisha ushirikiano.

(SAUTI YA MARK LYALL GRANT)