Ban awataka viongozi wa Senegal kuweka ushirikiano mbele

27 Machi 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa Senegal, anayeondoka madarakani Abdoulaye Wade, na Bwana Macky Sall ambaye anayeripotiwa kushinda katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma, kushirikiana kwa pamoja kwa maslahi ya watu wa taifa lao.

Bwana Ban amewapigia simu viongozi wote wawili akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Senegal kutokana na kuendesha uchaguzi huru na wa amani.

Katibu Mkuu Ban amempongeza Wade kutokana na kuridhia kushindwa kwake kwenye duru hilo la pili la uchaguzi, baada ya kuongoza taifa hilo kwa mihula miwili.

Ameelezea pia utashi mkubwa wa kisiasa ulioonyeshwa na kambi zote za kisiasa.

Ama amesifu kazi kubwa iliyofanywa na vyama vya kiraia akisema kuwa pande zote zimedhihirisha namna zinavyoweka zingatio la pekee kwenye uimarishaji mifumo ya kidemokrasia.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter