Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji kwenye kilimo utasaidia kutokomeza umaskini barani Afrika:UM

Uwekezaji kwenye kilimo utasaidia kutokomeza umaskini barani Afrika:UM

Umoja wa Mataifa umehimiza haja ya kuwekeza kikamilifu kwenye maeneo ya kilimo ikitaja kuwa ndiyo njia mujarabu ya kukabiliana na tatizo la umaskini barani afrika.

Kwa mujibu wa rais wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD, Kanayo F. Nwanze kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye eneo la kilimo ni hatua muhumu ya kufikiwa kwa malengo ya maendeleo ya millenia.

Amesema uwekezaji kwenye kilimo ndiyo njia muafaka na yenye uhakika hasa wakati huu wa kuelekea kwenye kilele cha ufikiaji wa malengo ya millenia.

Bwana Nwanze ameeleza hayo wakati akijiandaa kuhudhuria mkutano wa kimataifa utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia ukiwahusisha mawaziri kutoka barani afrika kwa ajili ya kupanga mikakati ya kusukuma mbele ukuzaji wa shughuli za kilimo.