Matumizi ya sheria yanaweza kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake:Manjoo

27 Machi 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo ametoa wito kwa serikali ya Papua New Guinea kutumia njia za kisheria kwenye harakati zake za kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake.

Akikamilisha ziara yake nchini humo Bi Manjoo pia ameushauri utawala wa nchi hiyo kuondoa baadhi ya itikadi za kitamaduni zinazowadhulumu wanawake.

Mtaalamu huyo amelitwika jukumu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza dhuluma dhidi ya wanawake, kinachosababisha dhuluma hizo pamoja na athari zake.

Manjoo amesema kuwa wajibu wa kuzuia dhuluma dhidi ya wanawake, kuwalipa fidia waathiriwa na kuwachukulia hatua wahusika  uko mikononi mwa nchi.

Kulingana na mtaalamu huyo  dhuluma dhidi ya wanawake huanza kutoka nyumbani  ambapo watoto wasichana na wanawake hujipata kwenye dhuluma za kimwili na kimapenzi.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter