IOM yawasaidia vijana kumaliza masomo yao nchini Ufilipino

27 Machi 2012

Mamia ya watu wamefaidika kutoka kwenye mradi uliozinduliwa miaka miwili iliyopita uliokuwa na lengo la kuwasaidia vijana wasiojiweza na watoto wa wahamiaji kwenye baadhi ya mikoa maskini zaidi nchini Ufilipino kumaliza masomo yao.

Mradi huo ulioanzishwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na chama cha wafilipino wanaofanya kazi mataifa ya kigeni ulitoa huduma za elimu kwa watoto wasiojiweza kwenye shule 15 za kitaifa zilizochaguliwa kwa kuwawezesha watoto kukaa shuleni, wapate elimu bora na ajira bora baadaye.

Maelfu ya vijana wa kifilipino hukosa kuendelea na masomo yao kutokana na ukosefu wa fedha suala ambalo huchangia wao kutopata ajira. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa habari wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud