Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapendekezo ya majina ya wagombea urais wa benki ya dunia yasitishwa

Mapendekezo ya majina ya wagombea urais wa benki ya dunia yasitishwa

Bodi ya wakurugenzi wakuu wa benki ya dunia imethibitishwa kwamba kipindi cha kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi ya urais wa Benki hiyo kimemalizika Ijumaa Machi 23.

Bodi hiyo ya wakurugenzi imesema ina furaha kutangaza kwamba majina matatu yatafikiriwa katika nafasi ya Urais ambayo ni Jim Yong Kim raia wa Marekani na Rais wa chuo cha Dartmoth New Hampshire, mwingine ni Jose Antonio Ocampo raia wa Colombia na profesa katika chuo kikuu cha Columbia hapa New York.

Na mgombea wa tatu ni Bi Ngozi Okonjo-Iweala raia wa Nigeria ambaye pia ni waziri wa uchumi na fedha wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taratibu wakurugenzi wakuu wa Benki ya dunia watawafanyia sahili wagombea hao watatu mjini Washington katika wiki zijazo na uchaguzi wa Rais mpya kwa njia ya maafikiano ya wote unatarajiwa kuwa katika mkutano wa majira haya ya kipupwe mwaka huu.