Vizazi vijavyo lazima vielimishwe kuhusu biashara ya Utumwa:Al Nasser

26 Machi 2012

Rais wa Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema biashara ya utumwa ilikuwa ni changamoto na mtihani kwa dunia na ili kukabiliana na changamoto kama hiyo unahitajika mshikamano, uwajibikaji, shiriki na ushirikiano wa kila aina katika jamii.

Akizungumza katika kumbukumbu maalumu ya kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashra ya utumwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Al-Nasser amesema ni lazima kuwe na ushirikiano wa karibu katika kuelimisha vizazi vijavyo kwamba utumwa katika mfumo wowote le ni suala lisilokubalika.

Ameongeza kuwa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashara ya transatlantic slave trade kunatoa fursa ya kuendelea kulishugulikia suala hili.

Amesema katika kufanya hivyo dunia itaelimishwa kuhusu hatari za ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine na kuhakikisha kwamba moja ya ukiukaji mkubwa kabisa wa haki katika historia ya mwanadamu hautosahaulika asilani.

Amesema watu wote tunapaswa kujifunza kutokana na ukatili na madhila hayo yaliyopita na kuhakikisha kwa kuchukua hatua zinazopaswa kwamba utumwa na mifumo yake yote imetokomezwa daima.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter