Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azuru Korea Kusini na kujadilia kitisho cha nyuklia

Ban azuru Korea Kusini na kujadilia kitisho cha nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na rais wa Korea ya Kusin Lee Myung-bak mjini Seoul.

Viongozi hao wawili walituwama katika eneo la mkwamo wa mambo huko Syria, urutubishaji wa silaha za nyuklia kwa usalama wa dunia na kinu cha Peninsula.

Ban ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya kikazi nchini kwake alikozaliwa, alirejelea tena kuelezea wasiwasi wake kufuatia tangazo la hivi karibuni la serikali ya Korea Kaskazini inayokusudia kuanzisha masafa ya satellite ambayo yanatiliwa mashaka na wengi.

Ameitolea mwito Pyongyang  kutafakari upya uamuzi huo na kusisitiza haja ya kuheshimiwa kwa azimio la Baraza la usalama linalopiga marafuku majaribio ya luteka za kijeshi .