Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan na Rais wa Urusi wakutana na kujadili hali ya Syria

Annan na Rais wa Urusi wakutana na kujadili hali ya Syria

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiaarabu Kofi Annan amewasili Moscow na kukutana na Rais Demitri Medvedev kujadili suala la Syria na njia za kumaliza matumizi ya nguvu na mauaji nchini humo.

Annan anajaribu kuishwishi Urusi ambayo ni mshirika muhimu wa Syria ichukue msimamo mkali dhidi ya Rais Bashar al Assad.

Katika mazungumzo yao Rais Medvedev ameonya kwamba ujumbe wa Kofi Anna uliotumwa Syria unaweza kuwa ni fursa ya mwisho ya kuepuka vita. Annan anasisitiza machafuko lazima yakome na suluhu ipatikane kwa njia ya amani. Ameishkuru Urusi na kusema atahitaji ushirikiano wake katika suala hili.

(SAUTI YA KOFI ANNAN)