Ban atoa heshima kwa wale wanaotetea ukweli na haki

26 Machi 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza mashujaa kote duniani kutokana na mchango wao katika kulinda haki za binadamu pamoja na kuhakikisha kuwepo ukweli na haki. Machi 24 ni siku ya kimataifa ya haki ya ukweli inayohusiana na ukiukaji wa haki za binadamu kwa minajili ya kuwakumbuka waathiriwa wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Pia siku hii imetengwa kwa kuwakumbuka wale wamejitolea maishani na waliopoteza maisha yao katika jitihada na kupigania haki za binadamu hasa mtetesi wa haki za binadamu Monsignor Oscar Arnulfo Romero aliyeuawa nchini El Salvador tarehe hii mwaka 1980 alipokuwa kwenye mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter