Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa UNHCR wawasili Kachin Myanmar na msaada wa dharura

Msafara wa UNHCR wawasili Kachin Myanmar na msaada wa dharura

Msafara wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ukiwa umesheheni msaada wa dharura wa kibinadamu umewasili eneo lililoathirika na vita la jimbi la Kaskazini la Kachin nchini Myanmar.

Msafara huo wa malori manne na magari madogo mawili umebeba matandiko, vyandarua vya mbu na vifaa vya jikoni, pamoja na chakula na misaada mingine kutoka mshirika mengine ya Umoja wa Mataifa.

Msaada huo ni kwa ajili ya watu 50,000 hadi 70,000 waliosambaratishwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Kachin tangu mwezi Juni mwaka jana kwenye mpaka kati ya Myanmar na Uchina.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)