Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka ulinzi kutolewa kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa

Ban ataka ulinzi kutolewa kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyataka mataifa yote kuungana ili kuwalinda maelfu ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaohatarisha maisha yao katika kuwasaidia wanaohitaji msaada kote duniani.

Ban amesema kuwa ni mataifa 90 yaliyoidhinisha makubaliano ya mwaka 1994 yanayohusu usalama wa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa huku nchi 27 zikiwa zimetia sahihi makubaliano ya mwaka 2005 yanayowapa ulinzi wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma za kibinadamu, kisiasa na kimaendeleo.  Ban ameongeza kuwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa ni waathiriwa wa visa vinavyohusiana na kukamata na kuzuiliwa, kutekwa nyara, dhuluma na pia mauaji.