Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yatoa ombi la kusaidia nchi za pembe ya Afrika

FAO yatoa ombi la kusaidia nchi za pembe ya Afrika

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO hii leo limetoa ombi la dharura la dola milioni 50 zitakazotumiwa katika kugharamia shughuli za ufugaji na kilimo kwenye pembe ya Afrika kabla ya msimu wa upanzi unaoambatana na mvua kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu.

Ufadhili huo utahitajika ili kufanikisha mpango wa siku 90 wa kuwapa wakulima na wafugaji njia za kuboresha maisha yao na kujiandaa kwa siku  za baadaye.

Kati ya programu zinazoendelea kwa sasa na zinazohitaji msukumo ni miradi ya kulipwa kwa kufanya kazi na uzalishaji wa mifugo.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)