Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaifuatilia kwa karibu hali nchini Mali:UNHCR

Tunaifuatilia kwa karibu hali nchini Mali:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafuatilia kwa karibu hali nchini Mali kufuatia tangazo kuwa wanajeshi wamechukua udhibiti wa nchi hiyo.

UNHCR inasema kuwa kumeshuhudiwa kuhama kwa wa watu  ndani mwa nchi au kwenda kwa mataifa jirani.

Suala linaloisumbua UNHCR kwa sasa ni  jinsi hali itakavyoendelea kuwa na iwapo inaendelea kusababisha kuhama kwa watu zaidi wakati ambapo idadi kubwa ya watu wamehama ndani na kwenda nje mwa Mali.

Maelfu ya watu wameikimbia mali tangu mwezi Januari kufuatia mapigano kati ya kundi la waasi na wanajeshi wa Mali kaskazini mwa nchi .

Watu waliohama makwao waanaishi kwenye mazingira magumu vijijini ndani mwa Mali wakiwategemea wenyeji.