Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan aelekea Moscow na Beijing

Annan aelekea Moscow na Beijing

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Kofi Annan anasema kuwa hana mpango wa kurejea tena nchini Syria na badala yake atachunguza majibu yaliyotolewa na nchi hiyo.

Annan anatarajiwa kujadili majibu yaliyotoka nchini Syria baada ya mapendekezo yaliyotolewa na katibu huyo mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ya kumaliza ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu unaondelea nchini Syria .

 Hata hivyo Annan anasema kuwa shughuli zake hazitazungumziwa kwenye vyombo vya habaria.

Ujumbe uliosafiri kwenda Syria ulikutana na maafisa wa ngazi za juu serikalini huku ukitarajiwa pia kukutana na rais pamoja na waziri wa mambo ya kigeni mjini Mexico.