Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna mabadiliko kwenye uongozi wa dunia:Ban

Kuna mabadiliko kwenye uongozi wa dunia:Ban

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kumeshuhudiwa nguvu na uwezo wa ushirikiano ambao umechangia kuleta matokeo duniani.

Akiongea kwenye taasisi moja nchini Singapore hii leo Ban amesema kuwa nchini Ivory Coast wito wa mabadiliko ulifanywa na  jumuiya ya uchumi ya mataifa ya magharibi mwa Afrika ECOWAS pamoja na Muungano wa Afrika.

Ameongeza kuwa nchini Libya mabadiliko yalifanywa kupitia ushirikiano wa mashirika ya kiislamu, Muungano wa Afrika na muungano wa nchi za kiarabu.

Ban aidha amesema kuwa huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya kisiasa katika karne ya ishirini na moja.

(SAUTI YA BAN)