Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washirikiana na Indonesia kuzindua mwongozo wa kukabili majanga ya dharura

UM washirikiana na Indonesia kuzindua mwongozo wa kukabili majanga ya dharura

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali ya Indonesia umezindua mwongozo maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wananchi wa nchi hiyo kukabiliana na majanga ya kimaumbile.

Mwongozo huo unaweka maelekezo na kutoa mbinu juu ya kukabiliana na majanga ya kimaumbile.

Unazingatia mpango wa miaka minne, kuanzia mwaka 2010 hadi 2014.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kitendo cha majanga ya dharura Valerie Amos ndiye aliyeongoza uzinduzi huo ambao pia ulihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali ya Indonesia.

Indonesia inatajwa kuwa ni miongoni mwa nchi duniani ambazo zinaandamwa mara kwa mara na majanga ya kimaumbile.