Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa afya wakaribisha azimio la usajili wa kuzaliwa

Wataalamu wa afya wakaribisha azimio la usajili wa kuzaliwa

Wataalamu wa masuala ya afya ikiwemo mtandao unatupia macho masuala ya afya pamoja na shirika la afya ulimwenguni WHO wamekaribisha azimio lililopitishwa na baraza la haki za binadamu linalozingatia usajili wa kuzaliwa.

Baraza hilo la Umoja wa Mataifa hapo jana lilipitisha rasmi azimio la ulazima wa kusajili uzaliwa kwa kila mtu kwa shabaha ya kupunguza kero zinazowaandama baadhi ya makundi ya watu.

Azimio hilo linaweka zingatia likitaka kila nchi mwanachama kuhakikisha anatekeleza kwa vitendo hatua ya kuwasajili wananchi na wakati huo huo likitupia macho haki ya kila raia.

WHO inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 hawasajiliwi kila mwaka.

Kuna vikiwazo vingi vinavyowabinya watu hao kutosajiliwa ikiwemo pia hali ya umaskini na kuishi maeneo ya mbali.