Iran imekiuka vikwazo vya silaha:UM

22 Machi 2012

Mkuu wa kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kufuatilia vikwazo vya silaha ilivyowekewa Iran kuhusiana na mipango yake ya kinyuklia imesema kuwa imepokea ripoti za ukiukaji wa baadhi ya vikwazo kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Kwenye ripoti yake ya kila miezi mitatu kati ya tarehe 21 mwezi Disemba mwaka 2011 na tarehe 20 machi mwaka 2012 balozi Nestor Osorio kutoka Colombia amesema kuwa mnamo tarehe 28 mwezi Februari nchi nne wanachama zilitoa ripoti za kuhusika kwa taifa la Iran kwenye shughuli zinazohusiana na makombora ya masafa marefu yaliyo na uwezo wa kubebeba zana ya kinyuklia.

Osorio pia amesema kuwa nchi moja mwanachama ilikuwa imeifahamisha kamati kuwa kuliingizwa nchini Iran vifaa vinavyotumika kwenye vinu vya kinyuklia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter