Ban aipongeza Malaysia kwa msaada wake kwa UM

22 Machi 2012

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelipongeza taifa la Malaysia kutokana na usaidizi wake kwa Umoja wa Mataifa na kulitaka kuendelea na moyo huo.

Akiongea wakati wa  chakula cha jioni anapondelea na ziara yake ya mataifa manne Ban amesema kuwa taifa la Malaysia limetoka mbali katika kuujenga uchumi wake akiongeza kuwa utajiri wa taifa hilo utawasaidia wasiojiweza kimaisha.

Ban amesema kuwa Malaysia ni mfano mwema katika kutimiza malengo ya milenia. 

Ban ataelekea nchini Singapore na kisha nyumbani kwao Korea kusini. Ziara ya Ban ilianzia nchini Indonesia mwanzoni mwa wiki hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter