Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha siku ya watu wenye matatizo ya kiafya

UM waadhimisha siku ya watu wenye matatizo ya kiafya

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya kimataifa duniani inayohusu matatizo ya kijeneti katika mwili wa binadamu.

Maadhimisho hayo ni hatua mojawapo ya kuhakikisha kwamba watu wenye matatizo hayo wanatendewa haki.

Hali hiyo inaweza kumfanya mtu kukosa mawasiliano ya moja kwa moja baina ya viungo vyake na akili.

Katika ujumbe wake kuadhimisha siku hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa watu wenye matatizo hayo ikiwemo watoto wameendelea kunyanyaswa na kubaguliwa