“Askari wanaoshiriki vitendo vya ubakaji wasipatiwe kinga”

22 Machi 2012

Mkuu wa shughuli za kipolisi kwenye Umoja wa Mataifa ametaka kukomeshwa tabia ya kukingiwa kifua kwa askari wa kulinda amani ambao mara nyingi wanatumbukia kwenye vitendo vya uvunjaji haki kama kushiriki kwenye matukio ya ubakaji na utesaji wa raia.

 Ann-Marie Orler,amewaambia waandishi wa habari kuwa askari wa kulinda amani ambao wanatumbikia kwenye matukio hayo lazima wafikishwe kwenye mkono wa sheria na kuhukumiwa kama taratibu zinavyosema.

Amezitolea mwito nchi wanachama kutowapatia kinga yoyote askari hao na wakati huo amezitaka kuchukua hatua za haraka kuzuia kutojitokeza tena kwa matukio ya jinsi hiyo.

Afisa huyo amesema ameanza kutiwa moyo kutokana na kuanza kupungua kwa matukio ya ubakaji na unyanyasaji, lakini ameongeza kuwa kunasalia visa kadhaa vya matukio ya aina hiyo ambavyo ametaka vikomeshwe.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter