Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kobler alaani mashambulizi ya mabomu Iraq

Kobler alaani mashambulizi ya mabomu Iraq

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amelaani vikali misururu ya mashambulizi kwenye miji kadha nchini Iraq ambapo watu kadha waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Martin Kobla amesema kuwa uhalifu unaotendwa kwa watu wa Iraq hautaruhusiwa ambapo amewataka wananchi wa Iraq kuwa macho na kukataa majaribio ya kuvuruga taifa lao na kuutaka utawala wa nchi hiyo kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa milipuko kadha ya mabomu iliyofuatana ilitokea kweye miji kadha ukiwemo mji mkuu Baghdad ambapo watu 40 waliuawa na wengi kujeruhiwa