Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani vikali mashambulizi kwenye shule ya Kiyahudi Ufaransa

Ban alaani vikali mashambulizi kwenye shule ya Kiyahudi Ufaransa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali matukio ya ufyatuaji risasi katika shule ya wayahudi Mjini Toulouse nchini Ufaransa ambako watu wanne walipoteza maisha ikiwemo watoto watatu.

Pamoja na kutuma salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huo, Ban amelishutumu shambulizi hilo akisema ni uharibifu wa hali ya juu.

Myahudi mmoja na watoto wake wawili walifariki dunia wakati wa shambulizi hilo ambalo pia lilififisha maisha ya mtoto wa mwalimu mkuu wa shule hiyo.