Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yataka kuongeza ufadhili kwenye kukabiliana na majanga

UM yataka kuongeza ufadhili kwenye kukabiliana na majanga

Kuna haja kubwa kwa makundi ya kihisani kutumia kwa kiwango kikubwa sehemu ya ufadhili wao kugharimia miradi itayopunguza maafa,  na wakati huo huo kuwafikia kwa wakati waathirika wa majanga.

Kulingana na ripoti moja iliyozinduliwa leo ambayo imeangazia suala la kudhibiti majanga, makundi mengi ya watu walioathiriwa na majanga ya kimazingira hayajahudumiwa vya kutosha.

Utafiti huo umebaini kuwepo kwa idadi kubwa ya watu ambao wanaendelea kutaabika kutokana na kuathiriwa na majanga.

Imetaka kubadilishwa kwa mkondo wa mambo hasa kwa kuzingatia anguko kubwa la kiuchumi linaloshuhudiwa kutokana na majanga hayo ya kimazingira

Inakadiriwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2009 kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3.7 ndicho kilichoenda kwa nchi maskini kufadhilia masuala yanayoangazia udhibiti wa majanga.