Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghan iko kwenye njia sahihi kuelekea kipindi cha mpito:UM

Afghan iko kwenye njia sahihi kuelekea kipindi cha mpito:UM

Shabaya ya kuifanikisha Afghanistan kuingia kwenye kipindi cha mpito bado inaendelea kupewa zingatio la pekee na Umoja wa Mataifa umehaidi kuendelea kuweka msukumo wake, pamoja na hali ya mikwamo ya hapa na pale iliyojitokeza hivi karibuni.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubis amesema kuwa kuna hali ya utengamano inavyojidhihiri sasa na hatua ya vikosi vya nchi humo kukabiliana na miwamo iliyozuka, inadhihiri namna taifa hilo lilivyotayari  kuendesha mambo yake.

Ameeleza kuwa juhudi zinandelea kufanywa wakati huu ili kuviongezea nguvu na weledi vyombo vya utoaji maamuzi, ikiwemo pia kuzipa mwanga mpya taasisi za utendaji ili hatimaye zitoe huduma bora kwa wananchi wake.

Hata hivyo ameyataka makundi ya korofi kujiweka kando na vitendo vinavyopalilia machafuko akisema kuwa huu sasa sio wakati wa kukumbatia vita.