Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza wananchi wa Guinea Bissau kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani

Ban apongeza wananchi wa Guinea Bissau kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Guinea Bissau  kwa kushiriki uchaguzi kwa njia ya amani uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Wagombea tisa akiwemo waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior na rais wa zamani Kumba Yala walishiriki kwenye uchaguzi huo uliondaliwa miezi miwili baada ya kifo cha rais Malam Bacai Sanha.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amewashauri wagombea pamoja na wafuasi wao kufuata sheria na kujitenga na vitendo vyovyote vinavyoweza kuzua vurugu.

Hata hivyo Ban amelaani mauaji ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini humo kanali Samba Djalo yaliyofanyika tarehe 19 mwezi huu ambapo aliutaka utawala kuwachukulia hatua wahusika.