Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu ahofia ghasia na usalama wa raia Guatemala

Mkuu wa haki za binadamu ahofia ghasia na usalama wa raia Guatemala

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay anahofia hali ya kusambaa kwa ghasia na usalama mdogo kwa raia uliosababishwa na ongezeko la mitandao ya uhalifu wa kupangwa, amesema naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang akitoa ripoti ya taifa hilo kwenye baraza la haki za binadamu Jumatano.

Bi Kang amesema watetezi wa haki za binadamu, watu wa asili na jumuiya ya wazee, pamoja na mazingira, vijana na wanaharakati wa haki za wanawake wamekuwa katika hatari ya kulengwa na ghasia kutokana na kazi zao.

Ripoti yake imerejea kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za kushughulikia matatizo ya usalama yaliyotajwa kutokea katika kampeni za uchaguzi mwaka jana, na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua muafaka kwa lengo la kutatua chanzo cha ghasia hizo.