Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzuia ghasia kabla hazijatokea ndio ngao ya UM:Ban

Kuzuia ghasia kabla hazijatokea ndio ngao ya UM:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuzuia ndio hisa za Umoja wa Mataifa katika biashara na ndio mwongozo katika miaka ijayo.

Ban ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa na usalama wa kimataifa, ushirikiano na ubia unaofanyika mjini Jakarta Indonesia, ukijadili ulinzi wa kimataifa.

Ban amesema wakati wa migogoro watu hawawezi kuangalia kando wakitarajia mambo yatakuwa mazuri.

Njia za kuchukua hata kuzuia mapema ghasia kabla hazijatokea ni suala la kulipa kipaumbele.

Amesema kwa maana hiyo ndio maana Umoja wa mataifa na wadau wengine wanajenga uwezo wa kutoa tahadhari ya mapema, kutafuta ukweli na njia muafaka ya kutatua migogoro kwa amani.

Ameongeza kuwa ndio maana wanapigania kuimarisha haki za binadamu, misingi ya demokrasia na sheria za kimataifa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)