IOM na washirika wawahamisha raia wa Mali walioko Niger

20 Machi 2012

Shirika la kimataifa  la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Niger pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wamewahamisha zaidi ya familia 500 kutoka Mali zilizokuwa zikiishi kwenye makao duni ndani na nje ya kijiji kilicho kusini magharibi cha Sinegodar.

Karibu watu 28,000 wakiwemo raia 4,500 wa Mali wamevuka mpaka na kuingia Niger kufuatia mapigano yanayoshuhudiwa nchini Mali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Tuareg.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter