Ubaguzi unachochea ghasia:Pillay
Utafiti mmoja unaonyesha kwamba machafuko mengi yaliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni yamechagizwa vikubwa na hali ya ubaguzi wa rangi.
Utafiti huo unasema kwamba wakati wa machafuko hayo makundi ya watu wachache hasa wahamiaji ndiyo yanayoathiriwa zaidi.
Kwa mfano utafiti huo umetaja machafuko yaliyotokea mwaka 2007 na 2009 kuwa ni kielelezo sahihi kinachoeleza namna haki za watu zilivyopuuzwa.
Akijadilia hali hiyo kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuendelea kuacha mienendo ya kibaguzi kunatoa tishio kubwa la kuzuka kwa machafuko.