Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maji Palestina kufuatia uvamizi wa chemichemi kutoka kwa walowezi:UM

Ukosefu wa maji Palestina kufuatia uvamizi wa chemichemi kutoka kwa walowezi:UM

Mamia kwa maelfu ya wapalestina wamekosa vyanzo vya upataji  maji  kufuatia uvamizi uliofanywa na walowezi wa Israel ambao wamehodhi vyanzo vyote vinavyotoa maji katika eneo la ukingo wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UM vyanzo vingi vya maji sasa vinashikiliwa na wahamiaji wa Israel, na idadi chache ya vyanzo hivyo vipo kwa wapalestina.

Katika ripoti yake juu ya hali jumla katika eneo hili shirika la UM linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA limesema kuwa hali hiyo pia imeharibu shughuli zingine za kimaendeleo.

Asilimia kubwa ya wapalestina wameanguka kutokana na kuendelea kukosa huduma ya maji.