Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi:Pillay

Hatua zimepigwa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi:Pillay

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa kugunduliwa kwa ugonjwa wa ukimwi miaka 30 iliyopita ni suala lililoushutua ulimwengu.

Pillay anasema kuwa  watu walishikwa na hofu ya kuambukizwa maradhi hayo kwa kumguza mgonjwa au kwa kupumua hewa moja hali iliyosabaishwa kufukuzwa kwa watoto shuleni, kufutwa kwa watu kazini  huku wengine wakishindwa kupata ajira.

Hata hivyo Pillay anasema kuwa miaka 30 baadaye maambukizi ya virusi vya ukimwi yamefikia viwango vya chini zaidi tangu ugonjwa kufika kileleni.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)