Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa misaada kwa wakimbizi wa Mali walioko eneo la Sahel

UNHCR yatoa misaada kwa wakimbizi wa Mali walioko eneo la Sahel

Shirika la  kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa usaidizi kwa maelfu ya wakimbizi wa Mali wanaokimbia mapigano kati ya waasi wa Tuareg wa Mouvement National de Libération de l’Azawad  na wanajeshi wa Mali and  tangu mwezi Januari.

Tani sitini za misaada ikiwemo blanketi, matandiko na vyombo vya jikoni  vinasafirishwa kutoka kwa ghala la UNHCR lililo Accra Ghana kwenda nchini Niger pamoja na tani 52 kwenda nchini Burkina Faso.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)